Nyota wa muziki Augustine Miles Kelechi AKA Tekno Miles, kutoka Nigeria
Onyesho hilo ambalo litakuwa ni gumzo mjini litafanyika kwenye mkesha wa kuamkia mwaka mpya wa 2016 Jijini Dar es Salaam.
Tekno Miles anayetamba na video ya wimbo wake mpya 'Duro' ameweza kukutana na waandishi wa habari akielezea jinsi alivyojiandaa kwa burudani nzima aliyowaandalia mashabiki wake katika onyesho hilo kulifanya kwa mara ya kwanza kabisa katika aridhi ya Bongo.
Naye Gimel Androus Keaton aka Dj Guru alikuwa na machache ya kuongea kuhusiana na ujio wake nchini Tanzania akisema kuwa hii ni mara yake ya pili kukanyaga ardhi hii na anatarajia kutoa burudani kali akishirikiana na ma djs wa hapa nchini.