Sunday , 13th Sep , 2015

Mkali wa miondoko ya muziki wa dansi nchini anayeimbia bendi maarufu ya Akudo Impact Tarsisi Masela amekataa kata kuhusu uvumi wa baadhi ya mashabiki kusema kuwa anamuiga staa Christian Bella katika uimbaji wake.

staa wa muziki wa dansi wa bendi maarufu ya Akudo Impact, Tarsisi Masela

Hii ni baada ya Tarsisi kuanza kufanya kazi nje ya kundi lake la Akudo akiwa kama solo artist kwa kutoa wimbo wake unaoitwa usingizi na kuonekana kutaka kufuata njia zake Bella katika kutoa kazi zake binafsi nje ya kundi.

Hapa kupitia enewz Tarisi Masela aamua kuweka wazi juu ya uvumi huo.