Wednesday , 28th Oct , 2015

Mwanadada mahiri wa muziki wa injili nchini Subira Mkwabi ambaye ameanza kuchipukia katika muziki wa injili amewaomba watanzania kuiachia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye kazi yake na kuiombea amani.

msanii wa muziki wa injili nchini Tanzania Subira Mkwabi

Subira ambaye pia ni mwalimu ameiambia eNewz kuwa hivi sasa anatarajia kufanya makubwa katika muziki huo wa injili akiitambulisha albamu yake ya kwanza aliyoibatiza jina 'Bwana Sema Neno', na pia aelezea kuhusu wanamuziki nyota waliomvutia kuweza kusimama vyema katika muziki.