Saturday , 12th Sep , 2015

Mkali wa muziki wa R&B hapa Bongo, Steve R&B ameeleza kuwa moja ya sababu kubwa ya kupiga kimya katika game kwa muda, ilikuwa ni harakati za kuendeleza nafasi ya muziki wa R&B hapa bongo kwa kukuza kipaji kipya.

Steve R&B |Credoh

Baada ya kufanya kazi hiyo kwa muda, Steve anajivunia matunda kuanza kuonekana sasa kupitia nyota ambaye anamjenga, msanii wa muziki anayesimama kwa jina Credo.

Steve amesema kuwa, hatua hiyo inatokana na uchache wa wasanii wanaofanya vizuri katika mahadhi ya R&B hapa Bongo, wakati huo huo kukiwa na vipaji kibao mitaani ambavyo vinahitaji kuwekewa nguvu kupata nafasi ya kufanya na kusikika.

Steve R&B