Monday , 21st Dec , 2015

Mshereheshaji wa tukio la kumtafuta Miss Universe wa dunia ambaye pia ni mchekeshaji kutoka nchini Marekani Steve Harvey, ameaomba radhi kwa jamii baada ya kukosea kumtangaza mshindi na kumtaja mtu mwingine.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Steve ameandika juu ya msamaha huo, akiwaomba watazamaji wa tukio hilo pamoja na warembo, huku akidai ilikuwa ni bahati mbaya na kwamba anajisikia vibaya.

“Ningependa kuwataka radhi watazamaji kwa kuwakosea, ilikuwa ni kosa kweli, na pia ningependa kuwaomba radhi kwa moyo wote Miss Colombia na Miss Philipines kwa kosa langu, najisikia vibaya”, alisema Steve.

Steve Harvey alimtangaza Miss Colombia Ariadna Gutierrez Arevalo kuwa ni mshindi wa mashindano ya Miss Universe 2015, badala ya Miss Philipines Pia Alonzo Wurtzbach, ambaye ndiye ameibuka mshindi.

Mashindano hayo yalihusisha warembo 80 kutoka nchi mbali mbali duniani, huku Tanzania ikiwakilishwa na mrembo Lorraine Marriott.

Maneno aliyoyaandika Steve Harvey kwenye ukurasa wake wa twitter.