Friday , 2nd May , 2014

Msanii wa muziki Snura, ambaye umaarufu wake ulianzia katika sanaa ya maigizo, amekanusha taarifa za yeye kujiingiza katika muziki kwa nia ya kuwapiga madongo mahasimu wake.

Snura

Snura amesema kuwa, kuingia kwake katika muziki ni kutokana na uwezo wake katika sanaa, na pia muziki wake ni kwa ajili ya kutoa ujumbe kwa jamii na pia kuburudisha, tofauti kabisa na nia ya kutupia watu madongo kama ambavyo watu wengi wanavyokuwa wanatafsiri.

Tumeongea na Snura kuhusiana na ishu hii, na hapa mwenyewe anaweka mambo sawa sawa.