Monday , 7th Dec , 2015

Msanii Q Chief amesema pamoja na yeye kupata mafanikio makubwa kupitia muziki, ana mtoto wake wa kike ambaye ana kipaji cha muziki kumzidi yeye, lakini hataki ajiingize kwenye tasnia hiyo kwa sasa.

Q Chief ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kusema kwamba kwa sasa mtoto wake huyo inambidi asome kwanza, kabla hajajihusisha na muziki.

“Mtoto wangu wa kike anaimba sana, yani staki hata ajihusishe, ni muimbaji kuliko hata mimi, lakini sasa it's too early kwa yeye kuanza, mi nataka asome sitaki kumkatili elimu”, alisema Q Chief.

Q Chief ameendelea kusema kwamba yeye kama baba amepitia mambo mengi ambayo msanii mwengine hajapitia, lakini bado ana amini muziki anaoufanya utamlipa siku za baadae bila kujali kama atakuwa hai au ameshafariki.

“Mimi nimepitia situation kwenye muziki ambazo hamna mwanamuziki yeyote amepitia , bongo fleva has given me a chance to realise who i am, and what i worth, kwa sababu kila mtu anamzungumzia Q Chief, kwa nini asimzungumzie mwingine, that means i'm God of this music, and I believe one day it will pay me niwe hai au nimekufa”, alisema Q Chief.

Pamoja na hayo Q Chief amesema kuwa muziki alioufanya ni tofauti na muziki mwingine, kwa kuwa bado unaishi kwa ubora wake, na kwamba kuna baadhi ya wasanii humfuata kutaka kuzifanyia remix nyimbo zake.

“Mimi sikupiga muziki ambao ni buble gum, mi nimepiga muziki unaoishi kuliko maisha yangu, nikifa leo value yangu inakuwa mara tatu ya mimi kuwa hai, and therefore unaweza hata ukawasomesha watoto wangu na kuwaendeshea maisha yao, kwa sababu wengi wananifuata kutaka kupiga remix ya ngoma zangu, lakini naangalia anaenda kuiwaste au anenda kuitengeneza”, alisema Q Chief.

Mtoto wa kike wa Q Chief