Wednesday , 20th May , 2015

Nameless, star wa muziki kutoka nchini Kenya amekamata vichwa vya habari kwa mara nyingine na safari hii ikiwa ni baada ya kuonekana na silaha ya moto ambayo anamiliki.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Nameless

Picha hii ya Nameless imezua tena mjadala kwa kuwaacha wengi na maswali endapo kitendo cha kuonesha silaha hizo hadharani ambacho kimezoeleka sasa kwa watu maarufu ni sahihi na ni nini wanataka jamii ijifunze kutokana na hilo.

Mpaka sasa star huyo bado hajatolea ufafanuzi hatua yake hiyo ya kuonekana na silaha hiyo, wakati huo picha yake ikiendelea kusambaa na kujadiliwa kwa kazi kubwa mtandaoni.