Monday , 15th Feb , 2016

Sikukuu ya wapendandao imefanyika Jumapili ya tarehe 14 watu maarufu na mashabiki kila upande wamesherehekea sikukuu hii kwa mitindo tofauti.

Ben Pol

Sikukuu ya wapendandao imefanyika Juma pili ya tarehe 14 watu maarufu na mashabiki kila upande wamesherehekea sikukuu hii.

East Africa Radio na East Africa Television kwa ushirikiano mkubwa wa King Solomon Hall Kinondoni paliandaliwa Valentine Affairs burudani ya nguvu kabisa pamoja na chakula cha jioni kwa wapendanao walio fika siku ya wapendanao,

Mastaa wa muziki wa bongo fleva waliokuwepo kutoa burudani ni pamoja na Ben Pol, Grace Matata, Patricia Hillary mwana mama aliye tamba na vibao vyake matata kama Njiwa Peleka Salam na Mwali Bado Mdodo pamoja na Malfred kati ya wengi walipendezesha usiku huo, ukishereheshwa na watangazaji wakali kutoka EA Radio, Irene Tillya na Anorld Gosbert.