Msanii MR. Blue aliyeshika Mic akiwa pamoja na Abby Skills waliposhiriki FNL
Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa, Mr. Blue amesema anatambua umuhimu wa msanii kupata tuzo ila kwa bahati mbaya yeye hajawahi kupata tuzo.
“Mimi sijawahi kupata tuzo yoyote siyo ya kitaifa wala ya kimataifa ila ninachoamini mimi ni kwamba mimi ni ‘expensive’ na ndiyo maana natoa ngoma mara moja kwa mwaka na inadumu kwa muda mrefu” Amesema Mr. Blue
Aidha Mr. Blue ameongeza kuwa tuzo ambazo zimeanzishwa na EATV zitasaidia sana wasanii wengi kuweza kutambulika zaidi na anaamini pengine anaweza kupata tuzo hiyo na ikawa tuzo yake ya mara ya kwanza.






