Friday , 10th Mar , 2017

Msanii Barnaba Classic amesema hajaona manufaa yeyote katika muziki wake kwasasa kufanya ‘collabo’ na wasanii kutoka ng’ambo huku akisisitiza kuwa yeye ndiye anaongoza kwa kupiga ‘show’ nje ya Tanzania.

Barnaba Classic

Barnaba amesema anaogopa kwa kipindi hiki kufanya hivyo kwakuwa muziki wake bado ni mdogo hivyo anaendelea kuinua kidogo kidogo na endapo ataona umefika kule alipokusudia basi hana budi kufanya ngoma moja na msanii kuutoka ughaibuni.

“Muziki hautaki kubahatisha, mimi ni mwanamuziki ninayeongoza kwa kufanya ‘show’ nyingi nje ya nchi lakini sijataka kumshirikisha msanii yeyote wa nje kwa kuwa muziki wangu bado nauandaa, unaenda kidogo kidogo na nikiona umefika ninakotaka nitafanya hivyo”. Amesema Barnaba.

Kwa upande mwingine msanii huyo amesema yupo mbioni kuachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la ‘Lonely’.