Monday , 18th Jan , 2016

Kufuatia msanii Shetta kuonekana akiwa na gari ya kifahari Land Rover Discovery model mpya, gari ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi milioni shilingi 120 Tshs, amesema kuwa kwa sasa hataki kusema chochote kuhusiana na chuma hiyo hadi baadaye.

Shetta

Shetta ambaye bado haijafahamika wazi juu ya ni wapi anapotengeneza pesa zaidi na kupiga hatua za maendeleo kushinda watu wengine, kuhusiana na hatua yake hii kubwa ya kimaendeleo pengine na kutumia gari ya mamilioni ya shilingi, hiki ndicho alichokisema kwa mashabiki wake.