Friday , 3rd Jun , 2016

Mmiliki wa lebo ya Mj Record Master J amefunguka na kutufahamisha kwamba Msanii Shaa aliyekuwa akifanya kazi zake kupitia usimamizi wa lebo hiyo kwa sasa hasimamiwi tena kazi zake na lebo hiyo .

Star wa Bongo Fleva Shaa

Akizungumza na Enewz Master J alisema kuwa yeye huwa anasaini mkataba wa miaka mitano tu na msanii baada ya hapo msanii atakuwa tayari ameshatengeneza jina na mkwanja wa kutosha na hapo atakuwa anaweza kujisimamia mwenyewe kazi zake.

“Shaa hayupo tena Mj Record alisema siku hizi ana jina na mkwanja wa kutosha katika akaunti yake,alisema ataanzisha lebo atajisaini na kujisimamia mwenyewe ngoma yake ya sugua gaga ilimtengenezea mkwanja mrefu sana watu hawajui tu,

Pia Master J aliiambia Enewz kuwa hayo ni maamuzi yao tu ya kibiashara na si yakimahusiano yao ya kimapenzi pia sasa hivi anatafuta wasanii wengine wapya ambao ni chipukizi awasimamishe nao baada ya mwaka wapo fresh.