Friday , 17th Oct , 2014

Wasanii wa muziki kutoka Afrika Mashariki, Sauti Sol, Emmy Kosgei, Chameleone, Radio na Weasel, Eddy Kenzo na mchekeshaji Anne Kansiime wamechaguliwa kuwania tuzo kubwa za Black Entertainment, Film, Fashion, Television and Arts (BEFFTA).

Bien wa Sauti Sol

Wasanii hawa ambao wanakabiliana na ushindano mkubwa kutoka kwa wasanii wengine Afrika katika vipengele mbalimbali, wamepata nafasi hii baada ya kazi zao kutengeneza mashabiki wengi hususan katika bara la Afrika katika kipindi kifupi.

Tuzo hizi zinazogusa vipengele vyote katika upande wa Burudani, zinazoratibiwa na wadau kutoka Nigeria na zitafanyika tarehe 24 na 25 mwezi huu huko London UK.