Monday , 8th Feb , 2016

Msanii wa muziki Roma Mkatoliki ameamua kuhalalisha mahusiano yake na mama wa mtoto wake, akiwa sasa katika mchakato wa kuoa, mwishoni mwa wiki akikamilisha zoezi zima la send-off ya mpenzi wake huyo kuelekea harusi.

ROMA na mwenzi wake na wapambe wao katika Sendoff

Roma na Mama Ivan wamepata backup kubwa kutoka kwa msanii wa muziki Kala Jeremiah, ambaye alikuwa ndiye mpambe wa msanii huyo, akishirikiana na mwanadada ambaye mkali huyo wa ngoma kama Dear God, na Malkia amekana kuwa siye mpenzi wake.

Kuhusiana na mipango ya harusi, na mahusiano kati ya Kala na mrembo ambaye alikuwa mwenzi wa msanii huyo katika shughuli nzima ya upambe, usikose kutazama eNewz kesho jioni.

Tags: