
Real Jofu ameongea na eNewz kuwa ameungana pamoja na wasanii maarufu wanaofanya vizuri katika gemu ya muziki nchini wakiwemo Best Nasso, Stamina, Real Jofu Mwenyewe, Isaya Maua na Chief Maker ambao kati yao wanatarajia kuzindua kazi zao mpya katika show ya pamoja watakayotumbuiza Club House mjini Musoma Ijumaa ya tarehe 30 mwezi huu.
Aidha Real amewashukuru watanzania kwa sapoti yao kubwa waliyompa haswa baada ya kutoa video ya wimbo wake uitwao 'Wamenichagua' unaoendelea kufanya vyema kupitia stesheni mbalimbali nchini, amesema kuwa katika show hiyo iliyoandaliwa chini ya Thetocta Crew Kayombo, msanii Best Nasso atazindua video yake mpya iliyobatizwa jina 'Niko Bize'.