Sunday , 20th Dec , 2015

Rapa wa kike Nicki Minaj amedhihirisha kuwa yeye ni mbishi, baada ya kutumbuiza kwenye tamasha jana nchini Angola, licha ya wanaharakati wa haki za binadamu kukosoa tamasha hilo na kutaka lifutwe.

Rapa wa kike wa nchini Marekani Nicki Minaj

Rapa huyo ametumbuiza katika Jiji la Luanda katika hafla ya maandalizi ya Krismasi iliyoandaliwa na kampuni ya Unitel communications, ambayo kwa sehemu fulani inamilikiwa na familia ya kiongozi wa nchi hiyo rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye anadaiwa kujilimbikizia mali.

Rais Dos Santos, mwenye umri wa miaka 73, amekuwa akituhumiwa kwa kuhusika na rushwa, kutumia madaraka vibaya na kutishia wananchi wake, katika taifa ambalo limetumbukia katika lindi la umasikini, licha ya kuwa la pili kwa uzalishaji mafuta barani Afrika.