Tuesday , 18th Nov , 2014

Rapa Jaffarhymes ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa akiwa anakamilisha mwaka bila kutoa rekodi yoyote katika muziki, amesema kuwa hatua hii ni njia pia ya kuonyesha watu kuwa anaweza kuendesha maisha yake bila muziki.

msanii wa muziki wa bongofleva jaffaryhmes

Jaffarhymes amesema kuwa, yeye ni mfanyabiashara na pia msanii ambaye ni mkali na jina lake lilishajitengenezea nafasi yake katika gemu, tofauti na wasanii wanaotoka sasa hivi na rekodi za muda mfupi wakiwa wanajiona mastaa tayari.