Monday , 24th Nov , 2014

Balozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) kwa upande wa Tanzania, Rapa AY akishirikiana na watoto wapo katika mchakato wa kukamilisha rekodi yenye lengo la kufikisha ujumbe maalum kuhusiana na kundi hili kwa jamii.

msanii wa bongofleva nchini Ambwene Yesaya aka AY

AY amesema kuwa, anatarajia kuwa kazi hii itatoka hivi karibuni na kuwa na mchango mkubwa wa kufikisha sauti za watoto hawa kwa walengwa.

Msanii huyu amesema kuwa kutokana na kazi yake hii ya muziki anaweza kuwafikia watu wengi zaidi, na hii inamrahisishia zaidi kuongea na jamii na kutumia pia nafasi hii kuwafikishia ujumbe kuhusiana na masuala muhimu ya watoto.