Sunday , 23rd Mar , 2014

Msanii wa kundi la P-Square Paul Okoye, ameamua kufuata nyayo za pacha wake mkubwa Peter baada ya jana kuamua kufunga pingu za maisha na Mpenzi wake wa siku nyingi, na mama wa mtoto wake, Anita katika harusi ya kitamaduni huko Oga's Land Nigeria.

Vyanzo vya habari vimesema kila aliyeonekana na umuhimu mkubwa katika jamii nchini Nigeria alialikwa kuhudhuria harusi hiyo maridadi.

Nyota wa tasnia ya filamu nchini Nigeria nao hawakauachwa nyuma kwani alikuwemo Ini Edo pamoja na Omotola Jalade wakivalia sare za rangi ya Blue.