Tuesday , 2nd Sep , 2014

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Octopizzo ameweka wazi kuwa, safari yake barani Ulaya ambayo ilikuwa na lengo kubwa la kutangaza muziki wake, imekuwa ni ya mafanikio na kumuongezea kipato.

msanii wa nchini Kenya Octopizzo

Octopizzo amesema kuwa, ziara hii imefungua macho na kumpa michongo ya mbele huku akijitabiria mafanikio zaidi pamoja na safari nyingine katika bara hilo la Ulaya katika siku za karibuni.

Octopizzo amekuwa kwa muda huko Ujerumani ambapo amesema kuwa, imekuwa ni sehemu ambayo baada ya kufika alijisikia kama mtu ambaye tayari alikuwa huko kwa muda kutokana na muziki anaoufanya kukubalika.