Friday , 16th Oct , 2015

Msanii wa Hip Hop kutoka nchini Kenya, Octopizzo ameungana na harakati za kupambana na tatizo la ubakaji na ukatili kwa wanawake huko nchini Kenya, chini ya mpango wa Stop VAWG unaoendeshwa na taasisi maarufu chini ya serikali ya Uingereza.

Msanii wa Hip Hop kutoka nchini Kenya Octopizzo

Octopizzo ambaye atasimama kama balozi wa mpango huo ambao taasisi zake zipo sehemu mbalimbali duniani, leo hii ameshiriki katika uzinduzi wa kampeni dhidi ya ukatili unaofanywa dhidi ya jinsia ya wanawake ambayo imefanyika sambamba na burudani ya mchezo wa mpira wa miguu.

Hatua hii ni matunda ya mkutano kati ya Octopizzo na Sir Ciaran Devane ambaye ni mkuu wa kupitia taasisi ya elimu na mahusiano ya kiutamaduni - British Council huko London, ambayo ndiyo inayoendesha mpango huo.