Saturday , 9th Aug , 2014

Rapa Octopizzo kutoka nchini Kenya, anaendelea kuupandisha ngazi muziki wake ambapo sasa anajipanga kwaajili ya kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki wa kimataifa, DJ Mustard kutoka huko nchini Marekani.

Octopizzo

Octopizzo anatarajia kusafiri kwenda nchini London hivi karibuni kwaajili ya kukamilisha kazi hii kubwa, ambayo inatarajiwa kumuweka vizuri katika ramani ya kimataifa.

DJ Mustard anasimama na heshima kubwa katika game ya muziki kimataifa, sifa zake kubwa zikitoka katika utayarishaji wa ngoma kama Loyal ya Chris Brown, Rack City ya Tyga na nyinginezo.