Tuesday , 17th Nov , 2015

Nyota wa muziki Vanessa Mdee anayeendelea kung'ara kimataifa akiwa bado yupo nchini Nigeria aliposhinda tuzo ya Best African Pop ya AFRIMA, anatarajia kutumbuiza katika onesho la kimataifa la AMC huko Jo'Burg Afrika Kusini tarehe 21 mwezi huu.

Nyota wa muziki nchini Vanessa Mdee

Katika onesho hilo la aina yake, Vanessa atashiriki jukwaa moja na wasanii wakubwa kama vile Wizkid, Davido, AKA, Casper Nyovest, wasanii kutoka Cashtime Afrika Kusini, R2Bees, Flavour, Burna Boy na wengine wakali.

Onesho hili pia litahusisha wasanii wakali kutoka Afrika Mashariki akiwepo Chameleone pamoja na Viktoria Kimani likitarajiwa kuwa moja ya hatua kubwa kabisa katika historia ya muziki ya mwanadada Vanessa Mdee.