
Nuwa Wamala pamoja na washiriki wenzake, watatumia muda wa siku nne kutengeneza kazi ya sanaa ambayo itaambatanisha mtindo wa ubunifu na utamaduni wao, ili kupata ladha na mchanganyiko wa tamaduni mbalimbali za dunia katika sehemu moja.
Tamasha hili kubwa linafanyika kwa hisani kwa ajili ya lengo la kutangaza vivutio vya utalii kupitia sanaa mbalimbali, na kila msanii ambaye hushiriki, hupatiwa kazi maalum ya sanaa ya kutengeneza kwa kutumia ubunifu na uwezo wake katika sanaa hiyo.