Friday , 9th Oct , 2015

Msanii Mwasiti Almasi ambaye ni zao la THT, amesema alilazimika kuifanya mara mbili nyimbo ya sio kisa pombe ili kumridhisha Barnaba ambaye ndiye mtunzi wa nyimbo hiyo.

Mwasiti ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Frica Radio, na kufafanua kwamba wimbo huo ulikuwa ni wa mahadhi ya taratibu, lakini yeye alivutiwa na jinsi ambavyo Producer wake aliuutengeneza wa haraka.

"Nilikuwa naihofia sana kwa sababu ilikuwa ni kitu tofauti kidogo, kwa hiyo niliibadilisha vile nikaipeleka haraka, na kwa kutaka kumfurahisha Barnaba kuwa nilichokipokea nilifurahia ilifanya mbili, nilifanya slow na ile ya haraka", alisema Mwasiti.

Mwasiti aliendelea kwa kusema kwamba alipenda jinsi Quick Racka alivyo rap kwani alileta utofauti, na wimbo huo ni kazi ambazo hawezi akazisahau maishani mwake.