Friday , 17th Oct , 2014

Rapa Nikki wa Pili ameshauri kuwa, kuna umuhimu wa Maadhimisho ya siku za kitaifa kuwepo na mpango wa shughuli ama mambo ya pamoja ambayo watu kwa ujumla nchi nzima watakuwa wakiyafanya kuadhimisha siku hizi.

Nikki wa Pili

Nikki wa Pili amesema, kuna umuhimu wa nchi kuwa na utaratibu wa kuweka mambo haya ya pamoja yasiyopungua matano ambayo watu binafsi hadi taasisi watakuwa wakiyatekeleza ili kuleta maana zaidi katika siku hizi.

Rapa huyu amesema haya akizungumzia siku ya Nyerere ambayo kila mwaka imekuwa ikiadhimishwa kwa mapumziko na shughuli nyingine ambazo mwisho wa siku haziachi rekodi ya mafanikio fulani.