Monday , 2nd Jan , 2017

Rapa wa Bongo Nikki Mbishi amefunguka na kusema mwaka huu mpya wa 2017 ni mwaka mzuri kwake na muziki wake.

Rapa Nikki Mbishi na Solo Thang wakiwa katika studio za Fish Club

Hatua hiyo imekuwa zikiwa zimepita siku kadhaa toka rapa Fid Q amtaje Nikki Mbishi na Wakazi kama wasanii wa Hip hop ambao wanafanya vizuri kwenye muziki kwa kutengeneza kazi nzuri Ingawa anaona hawapewi nafasi licha ya kuwa na kazi nzuri na zenye tija

Nikki Mbishi alisema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram alipokuwa akionesha kukamilika kwa moja ya kazi yake ambayo amemshirikisha mkongwe wa muziki wa Hip hop nchini Solo Thang na kuwataka watu wakae mkao wa kusubiri kazi hiyo ambayo imetengenezwa na producer Lamar chini ya Fish Crab Studio. 
 
"2017 ni mwaka mzuri sana kwangu na nawaahidi makubwa cha muhimu pumzi na sala tu. Solo Thang ft Unju pia kuna tetesi za King Kiba kuwa kwenye 'chorus' au basi nisitoe sana siri za kambi" aliandika Nikki Mbishi 

Alikiba

Lakini pia mkongwe wa muziki wa Hip hop nchini Solo Thang alionesha kuwa amefurahia kukamilisha moja ya deni lake la kufanya kazi na Nikki Mbishi na kudai kuwa kwa sasa ana deni moja la kazi na Fid Q.

"Deni na Nikki Mbishi nimeshalimaliza, bado moja na ndugu yangu Fid Q twende kazi, nasuburi mwaliko" alisema Solo Thang