Thursday , 30th Oct , 2014

Rapa Ney wa Mitego, ameweka wazi kuwa ngoma yake maarufu ya Mwanamke Hapigwi ambayo aliiachia kipindi cha nyuma kidogo, ni kazi ambayo wazo lake lilikuja baada ya kushuhudia mama yake akipata kipigo kutoka kwa aliyekuwa baba yao wa kufikia.

Ney wa Mitego

Ney amezungumzia ngoma ya Mwanamke Hapigwi ikiwa wiki hii mama yake mzazi ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa, na kusema kuwa, ngoma hii ambayo ni maalum kwa wanawake wote duniani ikiwa pia inawazungumzia wanawake wale ambao wanapitia tatizo hili la ukatili wa kijinsia.