Madee ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa badala ya kuwepo kwa mawaziri hao, fedha ambazo zingetakiwa kulipwa mawaziri hao, zikatengeneze bara bara za juu maeneo ya Ubungo mpaka Manzese jijini dar es salaam.
“Ni mwezi kama na nusu hivi toka tumchague Mh. Rais lakini mpaka leo si unaona hatuna waziri yeyote yule na kila kitu kinaenda sawa, tofauti hata na mwanzo wakati tuna mawaziri, inawezekana kwa sababu ndani ya wizara husika kuna katibu mkuu, sasa yule katibu angeweza kuiendesha ile wizara husika pasipo kuwa na waziri”, alisema Madee.
Leo asubuhi msanii Madee alipost kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa kumbe hii nchi inawezekana kuendeshwa bila mawaziri.