Monday , 9th Feb , 2015

Star wa muziki Nazizi Hirji wa nchini Kenya, amejipatia shavu la kuwa balozi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Fahamu Afrika huko Kenya, inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya kuhakikisha uwepo wa haki katika jamii.

Msanii wa muziki wa nchini Kenya Nazizi Hirji

Kupitia nafasi hiyo, Nazizi ambapo atatumia nafasi na umaarufu wake kuwezesha shughuli za taasisi hii kufikia kwa wingi na kwa urahisi zaidi jamii, akiwa tayari amekwishaanza kazi katika ukanda wa Pwani ya Kenya kupitia kampeni iliyopatiwa jina 'Be The Voice' inayoendeshwa na taasisi hiyo.

Hii inakuwa ni nafasi nyingine kwa star huyu kuwa mfano mzuri na kuhamasisha jamii, baada ya kuwashangaza wengi hivi karibuni kwa muonekano wake mpya akiwa amepunguza unene na uzito kwa kiasi kikubwa.