NAZIZI
Wimbo huo ambao anategemea kuuachia siku ya wapendanao 'Valentine', umeanza kutangazwa na msanii huyo kwa namna ya kipekee ambapo ameweka matangazo ya wimbo wake huo kwenye mabango makubwa ya matangazo 'Billboards' kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa masanii yoyote nchini humo.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Naziz amejigamba kwa kuonesha kuwa yeye ndiye mwanamuziki pekee nchini kwao kuweka matangazo ya wimbo wake kwenye mabango makubwa barabarani, ikiwa ni ujio wake wa kishindo baada ya ukimya wa muda.



