Nay wa Mitego
Kauli hii imetoka kinywani mwa Nay wakati akijibu maswali ya mashabiki kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, baada ya kuchana mistari kadhaa iliyomo ndani ya ngoma yake mpya aliyoiachia leo mistari inayosema
Amesema kuwa kuwa yeye anatarajia kuwa mmiliki wa kanisa la imani anayoiamini yeye menyewe na kuongeza kuwa hiyo ni biashara inayolipa zaidi kwa sasa.
"Broo wewe kama una kiwanja chako jenga kanisa ni biashara inayolipa sana. Mimi natarajia siku za karibuni nitakuwa mmiliki wa kanisa kwa dini ninayoiamini mimi. Sitakuwa mchungaji lakini nitakuwa mmiliki wa kanisa" Nay aliwaeleza watazamaji wa KIKAANGONI.
Nay 'The true boy' ameongeza kwamba katika orodha ya matajiri kwa sasa barani Afrika ni viongozi na wamiliki wa makanisa.