Wednesday , 8th Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Nay Wa Mitego ametoa nafasi mbili kwa wasanii wa kike ambapo nafasi moja ikiwa ni ya muimbaji na nyingine ya msichana anayeweza ku'rap' ili amsajili kwenye lebo yake ya 'Free Nation'.

Nay wa Mitego

Akiongea kupitia eNewz Nay amesema "Nina mpango wa kumrudisha mkongwe mmoja ambaye alikuwa amepotea ila bado ana mashabiki wengi, japo huyu mkongwe anaendelea kutoa ngoma ila kuna vitu baadhi ambavyo vinakosekana kwenye muziki wake".

Hata hivyo Nay amesema kwa nafasi aliyoitoa ya akina dada haijalishi umri gani hata kama akuwa mzee anaweza kujiunga naye kikubwa awe na uwezo wa kuimba au ku-rap

Mtazame hapa akifafanua