Sunday , 9th Oct , 2016

Diva katika kiwanda cha filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameweka peupe hisia za moyo wake kuhusu kiu yake ya kupata mtoto wa kiume.

Kajala Masanja

Huyu hapa anafunguka: “Najua mtoto ni mtoto lakini kwa sasa natamani kuwa na mtoto wa kiume ili Paula naye ajivunie kuwa na kaka. Siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti na sasa tayari ninaye wa kike ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume,” alisema Kajala na kuongeza:

“Natamani kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia matumizi ya watoto wangu na kuipa familia matunzo bora.”

Kwa upande mwingine, Kajala ameweka wazi kuwa anatamani kuvuka nje ya nchi kimafanikio, jambo ambalo tayari kwa sasa limeanza kuonyesha dalili kwa kiasi kikubwa.

“Nataka kufanya sanaa ya kuvuka mipaka, nimejitahidi kadiri nilivyoweza ndiyo maana baadhi ya kazi zangu zimeanza kuvuka mipaka hasa kwa nchi za jirani zaidi zikiwa ni zile zinazozungumza lugha ya Kiswahili,” alisema Kajala.