Friday , 4th Dec , 2015

Msanii Aslay kutoka Yamoto Band amesema anataka muziki anaoufanya uwe chanzo cha biashara itakayomuingizia pesa na kuendesha maisha yake hata akiacha muziki.

Aslay ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa anafahamu atafikia umri ambao hataweza kufanya tena muziki, hivyo atahitaji kufanya issue zingine za kumuingizia pesa, lakini anataka muziki ndio uwe chanzo chake.

“Matarajio yangu ya baadae nifanye muziki nikifika umri ambao hauruhusu kufanya muziki niachane na muziki niwe na biashara yangu, niwe na maisha yangu lakini uziki huo ndio unifanye mimi niwe na maisha yangu, niwe na vitu ambavyo vinaweza vikanisaidia katika maisha yangu na wanangu baadae”, alisema Aslay.

Pamoja na hayo Aslay amewataka vijana kujituma na kujiajiri wenyewe, na si kungoja kuajiriwa kwani yeye anaona kuajiriwa ni utumwa.

“Vijana wengi nawaona wanajiajiri wenyewe ikiwemo mimi mwenyewe, ukiachana na mshahara wangu ninaoupata lakini kuna vitu ambavyo nafanya vinaweza vikaniingizia hela, lakini mi nawashauri vijana tuwe tunajiajiri wenyewe, ukitegemea kitu cha kuajiriwa ni kama utumwa”, alisema Aslay.