Thursday , 18th Jun , 2015

Msanii wa muziki Mzungu Kichaa ameeleza kuwa, kando ya muziki ambao unachezwa mara nyingi na kila siku katika vituo mbalimbali, kuna sekta muhimu kabisa ya muziki wa Live ambayo inakuwa kwa kasi na kuwakilisha nchi vizuri kitaifa na kimataifa.

Mzungu Kichaa

Staa huyu amesema hayo akiwa anatambulisha ujio wa project yake mpya kabisa 'Twajiachia' ambayo amefanya huko nchini Ujerumani, akishirikiana na mkali wa Reggae Malfred, video ya ngoma yenyewe ikiwa imeongozwa na Director Zeki Oguz Teoman wakati wa kurekodi kazi yenyewe katika jiji la Hamburg nchini Ujerumani.

Kuhusiana na kazi hii ambayo imezinduliwa rasmi usiku wa Jana, Mzungu kichaa amefafanua kuwa ni kazi yenye lengo la kuhamasisha kila mtu katika nafasi yake, kusherehekea mafanikio licha ya changamoto mbalimbali za maisha.