Sunday , 22nd Feb , 2015

Licha ya shughuli zake mbalimbali za kuisaidia jamii, Staa wa muziki Mwasiti Almasi ameweka wazi kuwa, kwa upande wake hata siku moja hajawahi kuifikiria siasa.

Mwasiti

Amesema hajawahi kufikiria kutafuta nafasi kwa upande wa kisiasa ili kuifanya kazi hiyo ingawa kuna kauwezekano ka kuchukua hatua hiyo hapo baadaye.

Mwasiti amesema kuwa, kwa sasa roho yake bado haijamruhusu kuchukua hatua hii, muda wake mwingi kwa sasa akiendelea kuutumia kwa kufanya muziki wake na shughuli nyingine za kijamii, na mwenyewe huyu hapa, anafafanua.