Friday , 26th Feb , 2016

Mzee Mapili alikutwa amefariki nyumbani kwake Tabata Matumbi. Inasemekana kifo chake kimejulikana usiku wa jana baada ya majirani kutomuona siku mbili nzima na kutia mashaka, ndipo walipoamua kuvunja mlango wa nyumba yake na kukuta mwili wake.

mwanamuziki mkongwe nchini marehemu Mzee Mapili

Majirani wa Mzee Mapili wamesema mara ya mwisho kumuona mkongwe huyo ambaye alikuwa akiishi peke yake nyumbani kwake, ni juzi ambapo waliangalia pamoja mtanange kati ya timu za Arsenal na Barcelona.

Shuhuda mmojawapo amesema mwili hauko katika hali nzuri, na jitihada za kuwatafuta ndugu zake zinaendelea.

Mzee Mapili alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kabla ya kifo chake.