Tuesday , 22nd Jul , 2014

Mwili wa mtoto wa kiume wa mwanamuziki wa Uganda Juliana Kanyomozi umetazikwa siku ya Ijumaa jioni huko Matugga.

mwanamuziki Juliana Kanyomozi wa Uganda

Salamu za rambirambi zimekuwa zikitumwa tangu mtoto Keron Raphael Kabugo afariki dunia katika hospitali za Aga Khan Jijini Nairobi baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa pumu.

Mwili wa marehemu Keron utawasili Uganda leo usiku, ukiambatana na Juliana pamoja na mzazi mwenzake Amon Lukwago ambao wapo Nairobi kuuchukua mwili huo.