Tuesday , 6th Dec , 2016

Shangwe za EATV AWARDS zimezidi kuwa kubwa na kufanya jiji zima la Dar es Salaam kuwa na habari moja tu ya tarehe 10 Desemba 2016 pale Mlimani City, ambapo historia itaandikwa katika tasnia ya sanaa Afrika Mashariki.

Tuzo hizo ambazo zimeibua hisia kubwa kwa wadau ni za kwanza kufanyika hapa nchini kwenye tasnia ya sanaa, hivyo wadau wameonekana wakizisubiri kwa hamu, huku wakijiapiza kutothubutu kukosa.

Haya ni baadhi ya maoni ya watu wanaosubiri kwa hamu siku ya tarehe 10, Desemba, 2016

 

Kubwa lililoibua shangwe zaidi ni pale EATV ilipomtangaza Salama Jabir ambaye ni kipenzi cha watu, kuwa HOST wa tukio hilo, huku wengine wakimuomba kuandika historia sambamba na tuzo hizo, kwa kuvaa vazi ambalo huwezi kumkuta Salama amelivaa, ambalo ni gauni.

 

Basi sawa..... tusubiri kutoka kwake, Je, ataandika historia na EATV kwa kuvaa gauni kwenye 'red carpet'!?