Msanii Ray C.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Ray C amewatakiwa watoto hao safari njema huku akiwasisitizia wamuamini Mungu kwani ndiye muweza wa yote, hivyo kama aliweza kuwanusuru kifo basi anawaponya na watarejea nchini salama baada ya matibabu.
Aidha msanii huyo ametumia pia siku hii kuwatakia kina mama wa watoto hawa heri ya siku ya mama duniani huku akiwatia moyo na kuwasisitizia wamuamini Mungu.
"Mtapona kwa nguvu ya Mungu kupitia madaktari, na mtarudi salama, ya Mungu ni mengi na tayari kashawaonyesha kupitia mliyopitia na bado mnahema, Happy Mother's day kwa wamama wote wa hawa watoto, Mungu azidi kuwaonyesha uwepo wake kwenu muda wote na mzidi kumuamini kuwa yeye ndio ngao ya maisha yenu" - Ray C.