.jpg?itok=Cvfpbv8E×tamp=1473319538)
Said fella ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa kama msanii hauna mamanagement nzuri au anaekumanage uko kwenye mahusiano nae, hauwezi kufanikiwa.
"Kama huna management nzuri au unakuwa na managent alafu anakuwa ndo bwana ako hauwezi kufanikiwa kwa sababu bwana ako nae anakuwa na ukomo, unaweza ukaitwa Mwanza bwana ako na yeye anataka aende, sababu unakuta mtu kiongozi wake ndio bwana ake, hata yule promoter anaemwita msanii wako mkoani unajua labda hataki muziki wake anataka akatembee nae tu, kwa hiyo vile vitu vinamuharibia msanii", alisema Said Fella.
Pamoja na hayo Said Fella amewataka wasanii wengine kutowakatisha tamaa wasanii wa kike pale kazi zao zinaposhindwa kufanya vizuri, badala yake wawaambie maneno ya kuwapa moyo wa kuendelea kufanya kazi.
"Unajua hawa kina mama mara nyingi wanapenda vitu vyao visikwame njiani, wanataka wakivuma waendelee kuvuma, hawataki wakutane na upepo mbaya, labda tuwashauri inabidi wakubaliane na hali yote, maana mtu anaweza akatoa nyimbo ya kwanza ya pili ya tatu, akitoa ya nne ikifeli anaanza kukata tamaa, kumbe unatakiwa kuendele kutoa nyingine, kwa hiyo kuna maneno ya kuwaambia", alisema Said Fella