Friday , 21st Feb , 2014

Rapa na mwanaharakati wa Hip Hop kutoka Marekani Yasiin Bey, maarufu zaidi kama Mos Def anatarajiwa kushiriki katika programu maalum inayojulikana kama Music Exchange itakayofanyika huko Afrika Kusini, kwa lengo la kuleta pamoja burudani ya muziki pamoja na filamu.

Mos Def ambaye pembeni ya muziki amepata mafanikio makubwa katika uigizaji filamu, ndiye atakayefungua programu hii ambapo atapata nafasi ya kuzungumza na washiriki kueleza uzoefu na ujuzi wake katika kuleta pamoja na kuwekeza katika burudani za Muziki na Filamu.

Programu hii itafanyika kwa siku mbili mfululizo katika jiji la Cape Town, kuanzia tarehe 7 na 8 mwezi Machi ambapo mbali na Mos Def, kutakuwa na wadau wengine mbalimbali wakubwa wa muziki na filamu kutoka sehemu mbalimbali duniani.