Monday , 1st Jul , 2019

Msanii wa Bongo Fleva na mkali wa hip hop nchini, Moni Central zone amezungumzia juu ya tuhuma kwamba yeye pamoja na mpenzi wake mwanadada 'Official Nai' kuhongwa saluni.

Moni Central Zone na mpenzi wake Official Nai

Akipiga stori na eNewz, Moni amesema kuwa hajui kama kuna stori kama hizo mtaani kwamba pesa zake hazifanyi chochote, anachojua ni kwamba yeye pamoja na Nai wanapambana kutafuta maisha yao bora kwa kutumia nguvu zao.

"Suala la kusema kwamba sijui kuna nani sijui nani, sijajua kwamba hizo hela zangu ninazotoa zinakwenda wapi. Lakini kwa taarifa tu ni kwamba hatuko mjini kwa ajili ya kulelewa, ni maneno ambayo yapo lakini tunafanya hivi kwa ajili ya kuhakikisha tunawahamasisha vijana", amesema Moni.

Kwa upande wake, Nai amesema kuwa watu wengi wanafahamu jinsi anavyopambana na akimsikia mtu anasema kuwa anahongwa, atamfanya kitu kibaya.

Mtanzame hapa akizungumza.