Ray C amewandikia ujumbe watu hao kwenye ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa anaumizwa na vitendo hivyo ambavyo vina lengo la kumharibia jina lake na kumtaka abaki kwenye hali aliyokuwa nayo ambayo anapigana kuacha.
“Seriously kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadam mwezangu anadiriki kuniharibia jina langu ili yeye apate kula! hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu? hiyo habari yani ni ujinga ujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwenye page yangu ya insta mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndio kwanza nahangaika kurudi tena kwenye kazi yangu”, aliandika Ray C
Ray C ameendelea kwa kusema kuwa watu hao wanaomuandika vibaya wana nia ya kumrudisha nyuma, bila kuangalia hatua alizopiga kwenye kupambana na maumizi ya madawa hayo.
“Mnajua kama mpaka sasa nimeshatoa vijana zaid ya sabini kwenye madawa na wako fit wanatumia methadone je mnajua hilo? hata siju moja sijawahi pata msaada wowote kutoka kwenu, huu mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa, its not easy but am a hard working woman, na ni mwanamke jasiri napambana na siogopi na kamwe sintorudi nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu” aliandika Ray C.


