Friday , 30th Jan , 2015

Leo Mkanyia, msanii na msomi wa muziki wa ladha laini wa kiswahili 'Swahili Blues', amesema heshima ya muziki ambayo ilikuwepo miaka ya 80 kwa taratibu imeanza kurudi, ikiwa pia ni juhudi na jukumu la wasanii kuendelea kushikilia asili ya muziki wao.

Mwanamuziki wa miondoko laini ya swahili Blues Leo Mkanyia

Mkanyia amesema kuwa, teknolojia ambayo iliingia miaka ya 90 imesababisha muziki wa Tanzania na heshima yake kushuka kwa kiasi kikubwa na kupoteza dira, jambo ambalo linahitaji kuendelea kufanyiwa kazi ili kurudisha muziki wa hapa nyumbani katika njia yake.