Friday , 27th Feb , 2015

Star wa muziki Mike Tee ambaye mbali na muziki anajishughulisha pia na biashara ya bidhaa zinazotengenezwa hapa hapa nchini, amejipatia shavu kuzishirikisha katika Tamasha kubwa la watu weusi huko nchini Australia.

Mike Tee amesema kuwa, amepata shavu hilo kutokana na kutumia mtandao vizuri kutangaza kile anachokifanya, akiwa na matumaini kuwa shavu hilo litasaidia pia vijana wengi na pia kutangaza bidhaa za kitanzania nchini Australia.