Monday , 30th Jun , 2014

Rapa Mike Tee kutoka katika mpango wake unaofahamika kwa jina Kitaa ambao una lengo la kusaidia wasanii kusambaza kazi zao mitaani, amesema kuwa utaratibu wa wasanii kutoa singo ili wafanye shoo ndio unaowasaidia kuendesha maisha yao.

Rapa Mike Tee wa nchini Tanzania

Licha ya kuwepo kwa malalamiko pia kuwa, kazi hizi za wasanii zinanyonywa na watu wa pembeni wakiwepo wale wanaochoma CD's na kuwauzia watu nyimbo kwa flash, Mike Tee amesema kuwa, yeye kupitia mpango wake wa Kitaa, anasambaza bure kabisa nyimbo za wasanii ili kuzitafutia nafasi ya promo, ila anafanya hivi kwa kazi za wasanii wale alioingia nao makubaliano maalum pekee.