
Msanii Jay Moe
Akizungumza na eNEWS Jay Mo alisema mara ya mwisho yeye kutoa video ya ngoma yake ilikua mwaka 2005 ngoma ambayo aliifanya na marehemu Albert Mangwea 'Mikasi'
Jay Moe anasema licha ya yeye kutotoa video hata moja zaidi ya mwaka mmoja lakini haijamuathiri chochote kama wasanii wengine kwasababu audio zake zinanguvu sana na bado anaendelea kupata show ambazo zinamuingizia mkwanja.